Bodi ya Wakurugenzi
Bodi ya Wakurugenzi
Bodi ya Wakurugenzi ya TBS ndiyo chombo cha juu cha usimamizi na utoaji wa mwelekeo wa kimkakati wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS). Bodi ina jukumu la kusimamia utekelezaji wa majukumu ya kisheria ya TBS, kuidhinisha sera na mipango ya maendeleo, kusimamia utawala bora, uwajibikaji na matumizi sahihi ya rasilimali ili kuhakikisha taasisi inatekeleza dhamira yake ya kulinda afya, usalama wa walaji, mazingira na kukuza ushindani wa bidhaa na huduma kupitia viwango na ubora.