SHIRIKA LA VIWANGO TANZANIA(TBS)
e-Services

Kamati za Kiufundi

 

Kiwango cha Tanzania hutayarishwa kwa kutumia Kamati za Kiufundi.Hadi sasa kuna kamati tisa (9) za usimamizi zinazofahamika kuwa ni kamati za (viwango) za Vitengo.Kamati za usimamizi zina takrimu wajumbe 12 kila mmoja.Wajumbe wanachaguliwa kutoka kwa wadau mbalimbali wakiwamo wa serikali, wanataaluma na utafiti, wazalishaji, wasambazaji na walaji.

Katika kila Kamati ya Kitengo kuna kamati za ufundi zenye wajumbe wasiozidi wanane (8) ambazo ni kamati za mabingwa kutoka kwa wadau kutoka kwa wadau mbalimbali.Wakati mwingine, kamati ya ufundi inaweza kuunda vikosi kazi vya kiasi cha walengwa 3 – 4 vinavyotayarisha rasimu ya awali. Kwa kawaida wenyeviti wa kamati zote huwa wanachaguliwa kwenye taasisi zisizo na upande wowote kama vile vyuo vikuu au kutoka Serikali na hasa inayohusika.Makatibu huchaguliwa TBS

Kamati ya Viwango ya Kitengo cha Kilimo na Chakula (AFDC)

Kamati hii ya viwango ya kitengo ina jukumu la kutayarisha viwango vinavyohusu teknolojia za chakula, usalama wa chakula ,mbolea (za kemikali) mazao ya kilimo, mifugo na bidhaa za mifugo, ufugaji kuku (ndege) na bidhaa na kadhalika.

Kamati hii inasimamia shughuli za kamati sita (6) za kiufundi zinazotunga viwango vya sekta ya kilimo na chakula.

1

AFDC 1

Usafi wa chakula na usimamizi wa usalama

2

AFDC2/5C2

Uwekezaji lebo, ufungashaji na vifungashio

3

AFDC 3

Ungaguaji sampuli na njia za upimaji

4

AFDC 4

Shahamu na mafuta

5

AFDC 5/5C5

Food addivites – viongoza chakula

6

AFDC 6

Lishe na vyakula kwa matumizi ya mlo maalumu

7

AFDC 7

Viwango, mimea ya upishi na vikotezo

8

AFDC 8

Mikoshiolojia (Kundi la ISO)

9

AFDC 9

Vifaa vya kulishia wanyama

10

AFDC 10

Mbolea na viboresha udongo

11

AFDC 11

Bioteknolojia

12

AFDC 12

Matunda na mboga vilivyosindikwa

13

AFDC 13

Vinywaji vyenye kilevi na visivyo na kilevi

14

AFDC 14

Maziwa na bidhaa za maziwa

15

AFDC 15

Pakuokea mikate, mandazi, keki (mapochopocho)

16

AFDC 16

Nafaka, jamii ya mikundekunde (kunde, choroko, njegere, maharage, dengu, soya, fiwi)

17

AFDC 17

Sukari na asali

18

AFDC 18

Chai

19

AFDC 19

Mbegu za Mafuta (oleaginous seeds)

20

AFDC 20

Tumbaku na bidhaa zake

21

AFDC 21

Vyakula vya wanga visivyo vya mafuta

22

AFDC 22

Nyama, kuku, mayai na bidhaa zao

23

AFDC 23

Samaki na bidhaa zake

24

AFDC 24

Kahawa na bidhaa zake

25

AFDC 25

Tathmini ya fahamu/hisia (sensory evaluation)

26

AFDC 26

Bidhaa za matunda na mboga zisizosindikwa

27

AFDC 27

Mabaki ya Dawa za mifugo kwenye vyakula

28

AFDC 28

Vyakula vilivyozalishwa kwa mbolea asilia

29

AFDC 29

Kakao na bidhaa za kakao

30

AFDC 30

Usambazaji mbegu

Kamati ya viwango ya kitengo cha kemikali na vifaa tiba (CDMC)

Kamati hii ya viwango ya kitengo ina jukumu la kutayarisha viwango vinavyohusu sabuni, ditajenti/visafishi, rangi, vinatilifu, viandikia na vifaa vinavyohusiana na bidhaa zote zilizotengenezwa kwa kemikali, dawa na vifaa tib ana vinginevyo.

Kamati hii inasimamia kamati za ufundi ishirini (20) zinazotunga viwango kwenye Nyanja za kemikali na vifaa tiba.

1

CDMC 1

Dawa za meno

2

CDMC 2

Sabuni na ditajenti/visafisha

3

CDMC 3

Vipodozi na bidhaa zinazohusiana

4

CDMC 4

Viberiti na fashifashi

5

CDMC 5

Bidhaa za kioo

6

CDMC 6

Ubora wa maji

7

CDMC 7

Kemikali za viwanda na maabara

8

CDMC 8

Dawa za kuulia wadudu wa vyumbani

9

CDMC 9

Gesi

10

CDMC 10

Viandikia na bidhaa na kapatasi

11

CDMC 11

Plastiki na bidhaa za plastiki

12

CDMC 12

Rangi na vanishi

13

CDMC 13

Mpira na bidhaa za mpira

14

CDMC 14

Petroli na bidhaa za petrol

15

CDMC 15

Dawa

16

CDMC 16

Vilainishi na bidhaa za oili

17

CDMC 17

Utunzaji wa nyumba, burudani na vifaa vya michezo

18

CDMC 18

Bioenergy

19

CDMC 19

Dawa asili

20

CDMC 20

Vifaa tiba

Kamati ya kitengo ya viwango vya Jumla (GDC)

Kamati hii ya viwango ya kitengo ina jukumu la kutayarisha viwnago kwa ajili ya masuala mtambuko ya kwenye uhandisi na teknolojia za uchakataji na kaitka tasnia ya huduma kama vile utalii, hoteli, uchukuzi/usafirishaji, elimu, shughuli za kijamii na nyinginezo. Viwango hivi vinakusudia kushughulikia mahitaji yanayojitokeza katika sekta ya huduma na kuwakilisha eneo linalokuwa/linaloendelea (growth area)

Kamati hii inasimamia shughuli za kamati nane (8) za kiufundi zinazotunga viwango vya viwango vya jumla vinavyotokana na masuala mtambuka katika uhandisi wa teknolojia ya uchakataji.

1.

GDC 1

Kiasi, vipimo, alama na mambo ya ubadilishaji

2.

CDC 2

Machujio/machekeche, uchekechaji na njia nyingine za kupata kiasi ……………. Majengo na ujenzi (hudding na construction)

3.

CDC 3

Usimamizi wa ubora na uhakiki wa ubora

4.

CDC 4

Ufungashaji

5.

CDC 5

Utunzaji taarifa

6.

CDC 6

Msaada kwa jamii (social responsibility)

7.

CDC 7

Huduma kwa jamii (societal security)

8.

CDC 8

Utalii na huduma zinazohusiana

Kamati ya viwango ya kitengo cha ufundi umeme (EDC)

Kamati hii ya viwango vya kitengo inatayarisha viwango katika uwanja wa uzalishaji nishati ya umeme, upelekaji, usambazaji na vifaa yva utumiaji, nyenzo za kuchenjua umeme, waya za kusukia, vifaa vya kupimia na kudhibiti mchakato na betrii za msingi nabetrii fuasi (primary and secondary battores).

Pia ni uwekaji viwnago kwenye Nyanja za vifaa vya elektroni na mawasiliano ya simu ikiwemo sekta ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA).

Kamati hii inasimamia shughuli za kamati za ufundi sita (6) zinazotunga viwango vya sekta ndogo za umeme, vifaa vya elektroni na mawasiliano.

1.

EDC 1

Vifaa vya umeme

2.

EDC 2

Umeme wenye nguvu ndogo Zaidi na uhifadhi wa umeme

3.

EDC 3

Vifunga umeme (electrical installation)

4.

EDC 4

Mifumo ya king’ora na usalama ya kielektroni

5.

EDC 5

Nishati ifadidifu

6.

EDC 6

Vifaa vya mawasiliano

Viwango vya migodi na madini

Kamati hii ya viwango ya kitengo inatayarisha viwango kuhusu ishilahi/msamiati, njia za kuchukua sampuli, njia za upimaji, kanuni za utendaji, uamshaji wa vipimo kamili kwa ajili ya bidhaa na huduma zinazohusu utafiti wa madini, uchimbaji na uchakataji.

Kamati hii inasimamia shughuli za kamati za ufundi tisa (9) zinazotunga viwango vya sekta migodi na madini.

1.

MMDC 1

Utafiti

2.

MMDC 2

Upangaji wa mgodi, shughuli na huduma

3.

MMDC 3

Fundi nguo na bidhaa zinazohusika

4.

MMDC 4

Vifaa vya mgodi na kubebea udongo

5.

MMDC 5

Mifumo ya kisasa ya kielektroni ya migodi (Advanced automated mining systems)

6.

MMDC 6

Mawe ya madini na makinikia

7.

MMDC 7

Vito, ufundivito, mawe ya vito, metali za thamani

8.

MMDC 8

Elementi za madin adimu

9.

MMDC 9

Uchakataji madini na vifaa

Kamati na viwango ya kitengo cha nguo na Ngozi (TDC)

Kamati hii ya viwango ya kitengo inatayarisha viwnago vya utembo, mjuzi, ugwe, Kamba, nguo na vitu vingine vilivyotengenezwa bidhaa za Ngozi, njia za upimaji na maana na istilahi/msamiati unaohusiana

Kamati hii inasimamia shughuli za uwekezaji viwango za kamati za ufundi zinazotunga viwango katika sekta ya nguo na Ngozi.

1.

TDC 1

Bendera

2.

TDC 2

Mavazi

3.

TDC 3

Nguo/vitambaa vya ndani ya nyum ba

4.

TDC 4

Uwekaji lebo (vyeo)

5.

TDC 5

Utaratibu wa kupata sampuli na njia za upimaji

6.

TDC 6

Utembo – usiopenya moto na kuzuia kusambaa kwake

7.

TDC 7

Utembo – pamba

8.

TDC 8

Nyuzi na Kamba zinazosokotwa

9.

TDC 9

Vitambaa/nguo za hospitali

10.

TDC 10

Vikingamimba vya kitabibu (mechanical contraceptives)

11.

TDC 11

Ngozi na bidhaa za Ngozi

12.

TDC 12

Nguo za ufundi

Kamati ya viwango ya kitengo cha umakanika na uhandisi wa metalajia (MMEDC)

Kamati hii ya viwango ya kitengo hutayarisha viwango vinavyohusu uhandisi wa makanika ikiwemo migodi, mabusela, vyomba vya kanjeneo, upoozaji na kiyoyozi, ushughulikaji nyenzo, mitambo ya kilimo, uhandisi wa kemikali na uhandisi mwingine wa jumla kama vile compressa, mitungi ya gesi, bana za gesi na oili, uchimbaji wa visuka vya maji, seti za pampu, zana na vifaa vya elimu.Pia kamati hii inatayarisha viwango katika uwanja wa metalajia na uhandisi wa metalajia ikiwemo metali za chuma na zisizo za chuma, aloi na bidhaa zao, wawe ya madini na madini kuhalibu, vitu vigumu, metalajia ya poda, upashaji joto metali, mpako wa kuzuia kutu, mipako ya metali na isiyo ya metali (isipokuwa rangi, pigment/rangi za asili na uwekaji enameli) mna kutambuza.

Kamati hii inasimamia shughuli za kamati za ufundi nane (8) zinazotunga viwango kwenye tasnia ya umakenika na metalojia.

1

MMEDC 1

Viwanja vya msingi

2

MMEDC 2

Metali na miundo

3

MMEDC 3

Mabomba na uunganishi

4

MMEDC 4

Vijenzi vya magari

5

MMEDC 5

Zana na vifaa vya kilimo

6

MMEDC 8

Pampu na vifaa kutiririshia

7

MMEDC 9

Mkaa wa majiko ya mkaa

8

MMEDC 10

Moto na kuzuia moto

Kamati ya viwango ya kitengo cha usimamizi wa mazingira (EMDC)

Kamati hii ya viwango ya kitengo inatayarisha viwango kwenye uwanja wa mazingiraafya na usalama kazini, usafi wa mfumo wa majitaka na usio wa majitaka na utakasaji majitaka.

Kamati hii inasimamia shughuli za kamati za kiufundi nane (8) zinazotunga viwango katika uwanja wa usimamizi wa mazingira.

1

EMDC 1

Majitaka

2

EMDC 2

Ubora wa Hewa

3

EMDC 3

Ubora wa Udongo/ardhi

4

EMDC 4

Usimamizi wa mazingira

5

EMDC 5

Kelele na mitetemo

6

EMDC 6

Mvurumisho

7

EMDC 7

Misitu

8

EMDC 8

Talea ngumu

Kamati ya viwanja ya kitengo cha ujenzi na uhandisi wa majengo (BCEDC)

Kamati hii ya viwango ya kitengo inatayarisha viwango katika uwanja wa ujeniz ikiwemo uhandisi wa majengo, vifaa vya ujenzi na ujenzi, ramani, usanifu, ujenzi na matengenezo ya majenog, kanuni za ujenzi na usalama wa majengo.Kamati hii pia inatayarisha viwango vya magogo ya mviringo, mbao zilizopasuliwa na mbao zilizochakatwa na nyenzo za mbao katika na kwa ajili ya matumizi yote, ikiwemo istilahi/usamiati, vipimo kamili na njia za upimaji. Viwango kuhusu muundo wa matumizi ya mbao, paneli za ubao, bidhaa nyingine za mbao pia kushughulikiwa na kamati hii.

Kaati hii husimamia shughuli za kamati za kiufundi kumi na tatu (13) zinanzotunga viwango katika tasnia ya uhandisi wa ujenzi, majengo na ujengaji.

1

BCEDC 1

Mchanganyiko wa mchanga na kokoto, mchanga na zenge/saruji

  • 2.

BCEDC 2

Uashi

  • 3.

BCEDC 3

Kanuni za ujenzi na majengo

  • 4.

BCEDC 4

Bidhaa za saruji, chokaa na za udongo wa mfinyanzi

  • 5.

BCEDC 5

Barabara

  • 6

BCEDC 6

Mbao zilizopasuliwa, magogo yaliyopasuliwa na vijenzi vya mbao

  • 7

BCEDC 7

Majengo ya usafi/ vyoo, vyombo vya usafi

  • 8.

BCEDC 8

Nyenzo za kuezekea na kumalizia

  • 9.

BCEDC 9

Madaraja na mifereji ya maji machafu/ bomba

  • 10.

BCEDC 10

Majengo ya mbao

  • 11.

BCEDC 11

Udongo kwa ajili ya madhumuni ya msingi na uhandisi ujenzi

  • 12.

BCEDC 12

Ujenzi na uhandisi, ujenzi kwa jumla

  • 13.

BCEDC 13

Milango na madirisha



Settings