SHIRIKA LA VIWANGO TANZANIA(TBS)
e-Services

Taarifa ya jumla

Kupima ustadi (PT) ni zana ya tathmini kwa utendaji wa maabara dhidi ya vigezo vilivyowekwa kabla kwa kutumia ulinganishaji wa maabara mbalimbali (ISO/ IEC 17043)

Mahitaji ya uthibitisho huru wa ustadi kutoka taasisi za usimamizi na wateja inamaanisha kuwa kupima ustadi ni muhimu kwa maabara zote za upimaji kwenye nchi zote. Ni sharti la utambuzi rasmi kwa ISO/IEC 17025 kwamba maabara ya shiriki kwenye mpango wa kupima ustadi, iwapo kuna mpango unaofaa kwa hiyo, pamoja na kutumia mbinu zilizohalalishwa kisheria, PT ni suala muhimu katika uhakiki wa ubora wa maabara.

Shirika la Viwango Tanzania kama Mtoaji wa PT

Mashirika ya viwango yote katika ukanda wa EAC yamepewa mamlaka na wajibu wa kutayarisha mipango ya kupima ustadi kama sehemu ya uboreshaji wa EAC SQMT. TBS kwa upande wake imekuwa miongoni mwa watoaji PT wa ulinganishaji wa maabara mbalimbali (ILC) ndani na nje ya kanda ya EAC.

Chini ya himaya ya mpango wa EAC PT, nchi wanachama wana huduma moja kwa mwaka inayohusisha matriki 21 ambapo TBS hutoa matriki 8 ambazo ni chumvi ya kula, mbolea, juisi ya matunda, asali, nondo, mabati ya kuezekea, paneli za sola na nyaya za umeme.

Matriki nyingine 13 zilizobaki zinatolewa na nchi wanachama kupitia mashirika yao ya viwango.

Jinsi ya Kushiriki

Mipango ya kupima ustadi (PT) huendeshwa kwa kuzipatia maabara zinazoshiriki sampuli za aina moja kwa upimaji kwa wakati mmoja. Maabara huchanganua sampuli hizo kama sehemu ya utendaji wa kawaida na kuripoti matokeo kwa mtoaji PT. Baadaye inapewa ripoti inayoonesha jinsi matokeo yao yanavyokubaliana na matokeo sahihi na pale inapolazimika wanaweza kuchukua hatua zinazofaa kuboresha utendaji.

Maabara zote zinazoshiriki zinapewa msimbo (code) kwa madhumuni ya utunzaji siri.

Gharama ya ushiriki katika mpango wa PT inatoa thamani nzuri ya fedha ikilinganishwa na athari za kutoa matokea yasiyo sahihi ambayo yanaweza kuhatarisha afya ya umma, kuharibu jina na sifa ya kampuni, kupata hasara au kukiuka kanuni za Taifa.

Kwa kawaida mzunguko wa EAC PT huanza na matangazo, mwezi Mei kila mwaka na kufuata usajili na mfululizo wa shughuli nyingine za PT ikiwemo utumaji wa sampuli kwa washiriki wote waliosajiliwa mwezi Septemba. Baada ya kuwasilisha matokea na tathmini, kutakuwa na ripoti za tathmini zilizotumwa Januari lakini ni washiriki waliolipa tu ndio watakaopata ripoti hizo. Mwisho wa kila mzunguko wa PT ambao mara nyingi unakuwa mwezi Machi kila mwaka, mashirika yote ya viwango hufanya warsha ya tathmini kwenye nchi mwanachama wa EAC yeyote, kwa washiriki wote katika matriki zote 21 kwa ajili ya maoni na kupanga kwa ajili ya mzunguko ujao.

Zingatia: gharama ya ushiriki katika kila matriki ni 220 USD kwa ajili ya parameta na vitendanishi vyote vilivyotajwa na kutakuwa na vitu vya ziada utakavyoomba na kulipia 50 USD na kuvitumia kama nyenzo za marejeo au udhibiti wa ubora. Kwa maelezo zaidi tafadhali pakua viambatisho vifuatavyo;

 

1.Brosha ya EAC (Brochure ya EAC)

eac brochure

2.Brosha ya matriki mpya (New Matrices Brochure)

new matrices brochure

3.Taarifa ya jumla ya EAC PT (EAC PT 2019 Part 1 Genera Information)

eac pt 2019 part 1 general information

4.Matriki za EAC PT (EAC Proficiency Testing Scheme Available Matrices)

eac proficiency testing scheme available matrices



Settings