SHIRIKA LA VIWANGO TANZANIA(TBS)
e-Services

Mpango wa Usajili Mifumo ya Usimamizi

Shirika la Viwango Tanzania (TBS) linatoa uidhinishaji mifumo ya usimamizi kulingana na masharti ya viwango yva kimataifa kwa kampuni za umma na za binafsi watengenezaji na watoa huduma wengine mawanda ya uidhinishaji mifumo ya usimamizi inahusu

 

ISO 9001

 

Mifumo ya Usimamizi wa ubora

 

ISO 14001

 

Mifumo ya Usimamizi wa Mazingira

 

ISO 45001

 

Mifumo ya Usimamizi wa Afya na Usalama kazini/mahala pa kazi

 

TZS 1770

 

Uchambuzi wa hatari na maeneo muhimu ya uthibiti

 

Manufaa ya uidhinishaji wa mfumo wa usimamizi

 

a. Kufanya kazi kwa ufanisi zaidi kwa kuwa michakato yako ypote itakuwa imepangwa na kueleweka na kila mtu kwenye biashara au shirika. Hali hiyo inaongeza tija na ufanisi kupunguza gharama za ndani.

b. Hutimiza masharti muhimu ya kisheria na usimamizi

c.Hupanuka kwenye masoko mapya, kwa sababu baadhi ya sekta na wateja wanahitaji ISO 9001 kabla ya kufanya biashara.

d.Hubainisha na kushughulikia mashaka ya inayohusiana na shirika lako.

e.Huboresha humjali mteja au kufahamu mchakato ndani ya kampuni

f.Huboresha dhamira ya usimamizi na kufanya uamuzi

g.Hali bora Zaidi ya kazi kwa kufanya kazi.

h.Huongeza motisha kwa wafanyakazi

i.Hupunguza ngharama za dosari za ndani na za nje

j.Kuendelea kuimarisha mifumo ya usimamizi wa ubora

k.Kuboresha takwimu/sifa ya kampuni

l.Huongeza imani ya mteja

 

Tafadhali fungua link zifuatazo kuona watoa huduma au Kampuni walioidhinishiwa Mifumo yao ya Usimamizi:

certified firms under iso 9001 2015 qms 2025 12 15

certified firms under iso 22000 2018 food safety management system 2025 12 15

certified firms under haccp 2025 12 15



Settings