SHIRIKA LA VIWANGO TANZANIA(TBS)
e-Services

UPIMAJI WA HIARI

Shirika la Viwango Tanzania (TBS) hutoa huduma ya Type Testing (TT) ambapo mteja kwa hiari yake huwasilisha sampuli kwa ajili ya upimaji kwa kutaka kujua ubora wake au kwa kujua ulinganifu wake dhidi kiwango husika

Hatua za kufuata:

  1. Mteja kuandika barua rasmi ya maombi kwa Mkurugenzi Mkuu wa TBS akiomba huduma ya Upimaji wa Hiari.
  2. Baada ya kupokelewa maombi, mteja hupatiwa nukuu ya gharama ya huduma na kutakiwa kuihakiki na kuithibitisha.
  3. Baada ya malipo ya huduma kukamilika, mteja huwasilisha sampuli kwa ajili ya upimaji
  4. Upimaji wa sampuli katika maaraba husika
  5. Kutoa ripoti ya upimaji kwa mteja


Settings