NEP
Makubaliano kuhusu Viwango vya Kiufundivya Biashara (TBT) na Taratibu za Usafi na Usafimemea (Phytosanitary) (SPS) yanawataka wanachama wa WTO kuanzisha Kituo cha Maelezo ya Taifa (NEP) kama njia ya kupunguza matatizo ya shughuli za kibiashara yanayowakabili katika kupata taarifa kuhusu kanuni za kiufundi, viwango na taratibu za kutathmini utimizaji viwango, zinazotumika kwenye bidhaa zao katika masoko ya Kimataifa.
Shirika la Viwango Tanzania (TBS) kama Kituo cha Maelezo cha Taifa kuhusu Vikwazo vya Kiufundi vya Biashara Tanzania
Kituo cha Maelezo cha Taifa (NEP) kinashughulikia taarifa kuhusu kanuni za kiufundi na viwango vinavyotumika au kupendekezwa kutumika na taratibu ya tathmini ya utimizaji viwango zinazotumika au kupendekezwa kutumika. Hutumia rasirimali zilizopo kwenye maktaba kujibu waswala ya wasafirishaji bidhaa nje ya nchi na waingizaji nchini Tanzania na nje ya nchi.
Kituo cha Maelezo kinawezesha shughuli za kuuliza masharti ya kuingia kwenye masoko ya wanachama wa WTO ili waweze kujitayarisha kutimiza masharti hayo. Kituo pia kinafanya shughuli zifuatazo;
a)Kupeleka taarifa za mapendekezo kanuni za kiufundi na taratibu za tathmini ya utimizaji viwango vya Tanzania kwa Sekretarieti ya WTO/TBT/SPS kupitia Wizara yenye dhamana ya Viwanda na Biashara
b) Kushughulikia maombi yanayotaka taarifa kutoka kwa wanachama wa WTO kuhusu viwango vya Taifa, kanuni za kiufundi na taratibu za kutathmini utimizaji viwango vya Tanzania.
c)Kushughulikia maombi yanayotaka taarifa kutoka jumuiya ya wafanyabiashara nchini Tanzania kuhusu viwango vya nchi za nje, kanuni za kiufundi na taratibu za kutathmini ni utimizaji viwango.
d) Kushughulikia maelezo kuhusu kanuni za kiufundi, viwango na taratibu za kutathmini utimizaji viwamgo na
e)Kupokea, kukusanya na kusambaza taarifa kuhusu TBT/SPS zinazotolewa na Sekretarieti ya WTO kwa wadau wa nchini Tanzania.
Wajibu wa Shughuli za Biashara katika Taratibu za Taarifa za TBT
Ufuatao ni wajibu wa shughuli za biashara katika taratibu za taarifa za TBI;
a)Kuchunguza kwa makini taarifa zilizosambazwa na TBT/SPS-NEP na kubainisha taarifa zinazoathiri bidhaa zao zinasafirishwa nje ya nchi.
b)Kuiarifu TBT/SPS-NEP kuomba nakala ya kanuni zizotajwa, kuzichunguza kwa makini na kutoa maoni kuhusu nakala ya kanuni zilizopendekezwa.
c)Kuishauri Serikali kuhusu masuala yanayotakiwa kupelekwa kamati ya WTO, TBT/SPS
d)Kuishauri Serikali kuhusu masuala ya utekelezaji wa makubaliano ya TBT/SPS
e)Kuhakikisha ushiriki wa kutosha kwenye vikao au mikutano ya Kamati ya TBT/SPS
f)Kuhakikisha kuwa mashirika yao mama yanaendelea kufanyakazi kwa ukamirifu na kwa vitendo na mtandao wa mawasiliano wenye ufanisi upo kwenye vyama mama kwenda kwa wanachama wao.
g)Kujadili masuala yanayohusu taarifa wakati wa mikutano, vyama vya biashara na kupeleka maoni yao serikalini
Kwa maelezo zaidi kuhusu masuala ya TBT, tafadhali wasiliana kupitia anuani ya baruapepe nep@tbs.go.tz au kamati ya Taifa ya TBT/ SPS katika Wizara ya Viwanda na Biashara.